Matthew 10:1-6

Isa Awatuma Wale Kumi Na Wawili

(Marko 3:13-19; 6:7-13; Luka 6:12-16; 9:1-6)

1 aNdipo Isa akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, naye akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, ili waweze kuwatoa na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila aina.

2 bHaya ndiyo majina ya hao mitume kumi na wawili: wa kwanza, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye; 3Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo; 4 cSimoni Mkananayo, na Yuda Iskariote aliyemsaliti Isa.

5 dHawa kumi na wawili, Isa aliwatuma akawaagiza: “Msiende miongoni mwa watu wa Mataifa, wala msiingie mji wowote wa Wasamaria. 6 eLakini afadhali mshike njia kuwaendea kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea.
Copyright information for SwhKC